GANOART PAGES

Arts of Tanzania Paintings

Arts and Culture from Tanzania, East Afrika

KUHUSU SANAA TANZANIA...

Tanzania imejaliwa kuwa na hazina mujarab ya wasanii na wabunifu.

 Sanaa na utamaduni wa Watanzania ni vivutio muhimu kwa sekta ya biashara, utalii na utafiti nchini kwetu. Tukiangazia michoro ya Kondoa Irangi ambayo ndiyo imeweka rekodi ya kuwa michoro ya kale zaidi ulimwenguni, inasadikiwa bila shaka kwamba ustaarabu wa mwanzo kabisa ulianzia pande hizo kutokana na utafiti uliofanywa kupitia michoro hiyo.  Watalii na wanunuzi wa sanaa duniani hutembelea ama huagiza sanaa na bidhaa za sanaa kutoka Tanzania kupitia njia mbalimbali.

 Baadhi ya majina makubwa na maarufu ya wasanii Tanzania ni kama Said Tingatinga [RIP], Agustino Malaba, George Lilanga [RIP], Prof. Elias Jengo, Philp Ndunguru [RIP], David Mzuguno [RIP], Hendrix Lilanga, Paul Ndunguru, Pandu, Imanjama, Thobias Minzi, Hajji Chilonga, Robino Ntila na wengineo wengi ambao sanaa zao zimeweza kufanya vizuri kwenye soko la ndani na kimataifa.

Kizazi cha wasanii kinaendelea kukua na sanaa imekuwa njia mahsusi ya uchumi kwa wanaoitegemea.

UNGA MKONO JUHUDI ZA WASANII KUJIAJIRI  

KARIBU ART PAGES ZA TANZANIA ARTS AND CRAFTS